Social Icons

Featured Posts

Thursday, February 28, 2013

MWANA FA ADAI KUWA SIRI YA MAFANIKIO YAKE NI MATUMIZI MAZURI YA VIPAJI ALIVYO NAVYO

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Hamis Mwinjuma 'Mwana Fa' aeleza, kuwa na kipaji zaidi ya kimoja ndiyo  sababu ya kipekee inayomtofautisha yeye pamoja na kazi zake na baadhi ya wasanii wengine wa muziki wa bongofleva


Aliyazungumza hayo jijini Dar es Salaam wakati akielezea mikakati yake aliyokuwa nayo ya kuiachia nyimbo yake mpya hivi karibuni inayoitwa 'Kama Zamani'ambapo mashabiki wake watapata fursa ya kuisikia nyimbo hiyo katika vituo vya redio mbalimbali nchini, alisema kipaji ndicho kinachompa fursa ya kufanya muziki katika ngazi ya kimataifa

Alisema muziki unamatawi mbalimbali kwani kuna baadhi ya wasanii wanakipaji cha kuimba tu lakini hawezi kufanya shoo katika 'stage' wapo baadhi wanajua kuandika na hawajui kuimba wapo wengine wanajua kufanya vyote kwa wakati mmoja

Akizungumzia kwa upande wake Mwana Fa alisema amejaaliwa kuwa na vipaji vyote kwa wakati mmoja huku akiwa na uwezo wa kuandika mashairi, kuimba pamoja na kulimiliki jukwaa pindi awapo katika shoo

"Nimejaliwa vipaji vyote hivyo, kwani nina uwezo wa kuandika mistari mizuri, kuimba na kulimiliki jukwaa na ndio maana shoo zangu zinakuwa na mvuto wa kipekee kutokana, sanaa na ubunifu niliokuwa nao "alisema Mwana Fa

Akizungumzia ujio wa wimbo wa 'Kama zamani' wenye mahadhi ya Hip Hop ambapo msanii huyo amewashirikisha baadhi ya wasanii kama Man'dojo, Domokaya na The Kilimanjaro Band (Wana Njenje), alisema kuwa ameamua kushirikisha wasanii hao ili kuleta radha tofauti ya muziki na mashabiki wapate muziki ulio bora

Alisema kuwa nyimbo hiyo italeta mabadiliko makubwa katika tasnia ya muziki kulingana na ubora uliopo, kwani imetengenezwa 'live' kinanda, gitaa vyote vinasikika kwenye muziki huo, chini ya mtayarishaji Pfunk Majani

CHOCOLATE ZAMPONZA WEMA SEPETU NA KUMFANYA APOTEZE "MENO"


CEO wa Endless Fame Films Wema Sepetu amelazimika kujisamilisha kwa daktari wa meno baada ya ulaji wa chocolate kumponza na hivyo kuozesha baadhi ya meno yake.

Kupitia Instagram, Miss Tanzania huyo wa zamani, ameshare picha akiwa kwenye clinic ya meno kung’oa jino lililokuwa likimsumbua.“Apparently I have 8 cavities…. oh god… does this mean no more chocolate for me,” ameandika. Kwa waliowahi kuumwa na jino wanaujua muziki wake, so get well soon Wema.


Wednesday, January 2, 2013

MASTAA BONGO WAMZUNGUMZIA SAJUKI

Hakika  tukio la kifo cha  nyota wa  filamu nchini Juma Kilowoko limewagusa wengi achili mbali wapenzi wa tasnia  hiyo ambayo kwa sasa  ndiyo imeshika  hatamu katika  ukanda wa nchi za maziwa makuu na kuelekea kwa kasi barani Ulaya
Hapo juu ni nukuu kutoka kwa watu maarufu wakitupia neno kuhusu kifo hicho

Tuesday, January 1, 2013

SAJUKI WA BONGO MUVI AMEFARIKI DUNIA

Simon Mwakifwamba (kushoto) na wadau wengine wakimsaidia Sajuki (katikati) kutoka jukwaani baada ya kudondoka katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha mwishoni mwa mwaka jana.

STAA wa filamu za Kibongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu. Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala, Rajabu Amiri ni kwamba hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen!
HII NI MOJA YA KAZI AMBAZO MAREHEMU SAJUKI  ALISHIRIKI

MKALI WA USWAZI ASIYEKUBALIKA KWA WATOTO WA 'KISHUA'

Kama utakuwa mfuatilia wa kweli wa muziki wa kizazi kipya Bongo,jila la Dullayo litakuwa moja ya majina ya nyota waliofanya poa katika gemu nadni 2012 kufuatia uwepo wa 'Hits Singel' zake nyingi ambazo kwa namna moja ama nyingine zimekuwa zikifanya poa  kwenye mitaa ya jiji la Bongo na nje ya jiji hili pia.

Taarifa kutoka uchunguzi uliofanywa na  MCHOMVUINK  zinasomeka kuwa Dullayo si mmoja wa wakali wanaotajwa  kwenye mitaa ya watoto wa 'Kishua' kama anavyosomeka  uswazi jambo ambalo limekuwa likishangaza wengi kiasi cha kuzani kuwa huenda hiyo ndiyo sababu ambayo imekuwa ikimfanya kutokujumuishwa  kwenye shoo mbalimbali kubwa ambazo huwakutanisha 'Oooh mama' ambao wengi wao hukutana BBM na Instagaram a.k.a (watoto wa Kishua).

Kufuatia uwepo wa tetesi hizo blog hii ilimasaka na hii ndiyo nukuu kutoka kwake  " siyo kweli kwamba mi nakubalika zaidi uswazi tofauti na mitaa ya watoto wa kishua, kilichopo ni kuwa kila kitu kinakwenda kwa wakati ninachoamini mimi ni kuwa nafanya poa kila sehemu ndiyo maana hata hao unaowaita watoto wa kishua wanasikiliza ngoma zangu, ni wakati tu ukifika utaniona kwenye shoo hizo kwa sababu pia huwa naagalia zaidi maslahi yangu sifanyi shoo ili mradi shoo" alisema Dullayo.

SIKILIZA  MOJA YA NGOMA ZA DULLAYO  HALAFU SEMA YAKO KUPITIA COMMENTS
 

Monday, December 31, 2012

KICHUPA KILICHOFUNIKA YOUTUBE HIKI HAPA


Hii ndiyo video ambayo imefunika zote katika mtandao wa youtube baada ya kupata watazamaji zaidi ya Bilioni Moja huku pia ikiongoza kwa kuchezwa zaidi katika vituo vya runinga huko Uingereza na pia kwenye nchi kadhaa za Asia.

Sema nayo kimtindo na utoe Comments zako

BATA, BATANI NA DMM 88.5 PANDE ZA KISAKI

Huu ni wakati ambao utaendelea kubaki kama kumbukumbu muhimu kwenye historia ya Clouds Fm, ilikuwa ni ziara poa ambayo imefanikisha mambo mengi na kuifunza mengi yanayoihusu nchi yetu.

  SOO KAM AULIKOSA ENJOY KWA VIDEO HIYO....

HII NDIYO INTERVIEW KALI 2012

Kama  ulikuwa msikilizaji mzuri wa  kipindi cha XXL  kutoka  hapa mjengoni 88.5, kuna  interview kibao ambazo zilifanyika  ndani ya siku 365 za 2012, ingawa  kwa mtazamo wako inaweza ikawa siyo hii lakini kama ambavyo mwenyewe nimechagua  kulingana na vigezo nilivyonavyo navyo mimi hii ndiyo interview bora kwa kipindi chote.
  Sema  chochote kupitia  uwanja wa Comments hapo chini....Baliidah..nitakuelewa tu.