Social Icons

Tuesday, January 1, 2013

MKALI WA USWAZI ASIYEKUBALIKA KWA WATOTO WA 'KISHUA'

Kama utakuwa mfuatilia wa kweli wa muziki wa kizazi kipya Bongo,jila la Dullayo litakuwa moja ya majina ya nyota waliofanya poa katika gemu nadni 2012 kufuatia uwepo wa 'Hits Singel' zake nyingi ambazo kwa namna moja ama nyingine zimekuwa zikifanya poa  kwenye mitaa ya jiji la Bongo na nje ya jiji hili pia.

Taarifa kutoka uchunguzi uliofanywa na  MCHOMVUINK  zinasomeka kuwa Dullayo si mmoja wa wakali wanaotajwa  kwenye mitaa ya watoto wa 'Kishua' kama anavyosomeka  uswazi jambo ambalo limekuwa likishangaza wengi kiasi cha kuzani kuwa huenda hiyo ndiyo sababu ambayo imekuwa ikimfanya kutokujumuishwa  kwenye shoo mbalimbali kubwa ambazo huwakutanisha 'Oooh mama' ambao wengi wao hukutana BBM na Instagaram a.k.a (watoto wa Kishua).

Kufuatia uwepo wa tetesi hizo blog hii ilimasaka na hii ndiyo nukuu kutoka kwake  " siyo kweli kwamba mi nakubalika zaidi uswazi tofauti na mitaa ya watoto wa kishua, kilichopo ni kuwa kila kitu kinakwenda kwa wakati ninachoamini mimi ni kuwa nafanya poa kila sehemu ndiyo maana hata hao unaowaita watoto wa kishua wanasikiliza ngoma zangu, ni wakati tu ukifika utaniona kwenye shoo hizo kwa sababu pia huwa naagalia zaidi maslahi yangu sifanyi shoo ili mradi shoo" alisema Dullayo.

SIKILIZA  MOJA YA NGOMA ZA DULLAYO  HALAFU SEMA YAKO KUPITIA COMMENTS
 

3 comments:

  1. kilichoandikwa hapo ni kweli kabisa, jamaa ni mkali san alakini kwenye hizo mashoo zao huwa hawamuiti sijui kwanini F**k u c****s fm

    ReplyDelete
  2. sio kiviiiiiile
    mi najua kawapa ki2 kidoogo
    na wewe Adam huwa unampa xana promo
    af niliskia
    jamaa ile ngoma ya naumia roho aliiba huko iringa

    ReplyDelete
  3. Ngoma ra ukweeeri k'nowmer yani mpaka bhax

    ReplyDelete