Lina
mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya Bongofleva kutoka kundi la THT
akicheza na Tausi mmoja wa mashabiki waliojitokeza katika tamasha la
Serengeti Fiesta 2012, linalofanyika kwenye uwanja wa Samoramjini Iringa ambapo wasanii mbalimbali wanafanya vitu vyao jukwaani
wakiburudisha mashabiki wa mkoa wa Iringa, Lina ameweza kufanya mambo
makubwa na kuwaimbisha mashabiki wake ukizingatia kwamba anatoka mkoa
huo
Meneja
Masoko wa kampuni mya Push Mobile Rugambo Rodney akitangaza washindi
wawili wa pikipiki walioshinda habati nasibu hiyo katika tamasha la
Serengeti Fiesta 2012 mjini Iringa kwenye uwanja wa Samora huku wasanii mbalimbali wa muziki wa Bongofleva
wakionyesha uwezo wao katika muziki na kukonga nyoyo za mashabiki
waliofurika kwenye uwanja huo, katika picha aliyeshika kipaza sauti ni
mtangazaji wa Clouds Fm, B12.
Meneja
Masoko wa kampuni mya Push Mobile Rugambo Rodneyakipiga picha ya pamoja
na mmoja wa Ali Mohamed Sanga kazi wa Msindo Iringa mjini ambaye ni
mshindi wa moja ya pikipiki
Amini akiimba jukwaani katika tamasha hilo
Mkali wa muziki wa R&B Ben Paul akikamua jukwaani kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.
Msanii
Rich Mavoko akiwa ameruka hewani wakati akicheza pamoja na wanenguaji
wake jukwaani katika tamasha la Serengeti Fiesta mjini Iringa.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya Linex akiimba kwa hisia kali jukwaani katika
onesho la muziki la Serengeti Fiesta kwenye
uwanja wa Samora mjini Iringa , msanii huyo mwenye uwezo wa kutawala jukwaa amefanikiwa kukata kiu ya mashabiki wa muziki wake.
Wadau
kutoka duka maarufu la nguo mjini Iringa wakishoo Love katika tamasha
la Serengeti Fiesta 2012 kwenye uwanja wa Samora mjini
Iringa ktoka kulia ni Sadok aka Isadow, Eric aka Ricrose na Gasper aka G
Star, duka lao linaitwa Perfect Classic Wear .
Shabiki wa muziki wa bongofleva anayejulikana kwa jina la Tausi akicheza na rafiki yake vilivyo katika tamasha hilo.
Dj
PQ akifanya vitu vyake kwenye mashine wakati wasanii wakiimba jukwaani
kazi yake kubwa ni kucheza CD za wasanii hao wakati wakiimba jukwaani.
Rachel akimwaga mauno jukwaani ametisha kwa ujumla mjini Iringa na mashabiki wamemkubali.
Msanii Sundy Gaga akifanya vitu vyake jukwaani katika tamasha la Serengeti uwanja wa Samora
Mshindi
wa Serengeti Fiesta Super Nyota kutoka mkoani Mbeya anayejulikana kwa
jina la Ney Lee akiimba jukwaani kwenye onesho la Serengeti Fiesta
linalofanyika kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongofleva anayekulikana kwa jina la Young Killer akifanya vitu vyake jukwaani huku
Hapa ni Full Kushangweka mwenye kurusha juu ngua haya, mwenye kitambaa mkononi haya mwenye koti haya ilimradi burudani imekolea.
Nyomi la mashabiki waliofurika kwenye uwanja wa Samora kwa ajili ya kushuhudia tamasha la Srengeti Fiesta 2012 mjini Iringa.
Wasanii
chipukizi kutoka mkoani Iringa wakiimba jukwaani katika shoo ya
utangulizi kabla ya wasanii maarufu kupanda jukwaani katika tamasha la
Serengeti Fiesta linalofanyika kwenye uwanja wa Samora mjini
Iringa.

Mashabiki wakifuatilia kwa karibu wakati wasanii chipukizi kutoka mkoani Iringa wakifanya vitu vyao jukwaani.

Mashabiki wamejitokeza kwa wingi ili kushuhudia kitakachofanyika katika onesho hilo ni full mzuka kwenye uwanja wa Samora

Msanii huyu naye alimekamua vilivyo jukwaani
No comments:
Post a Comment