Mkali wa michano kutoka kundi la Mtanashati Entertainments lililo chini ya Ostaz Juma Namusoma lenye maskani yake pande za Migomigo (Magomeni) jijini Dar, Dogo Janja, amesema kuwa ameamua kumpisha msanii mwigine kutoka ndani ya kundi hilo anayekwenda kwa jina la Amazon ili aweze kufanya vizuri hewani hivi sasa.
Akizungumza na mchomvuink mapema leo , Dogo Janja amesema kuwa ameamua kumpisha Amazon kama sehemu ya utaratibu uliowekwa na kundi hilo kila linapokuja suala la kutoa nyimbo mpya ili kuipa nafasi ngoma yake ya ‘Mamito’ iliyopo hewani kwa sasa.
“Nimeamua kumpisha Amazon, lakini binafsi natarajia kutoa ngoma yangu mapema mezi januari sambamba na PNC pia kazi ambazo tunazifanya hivi sasa kupita mikono ya Marco Chalie, soo fans wangu wakae mkao wa kula na wasihtushwe na ukimya huu kwa ni ni utaratibu tu uliopo ndani ya kundi” alisema Dogo Janja