Social Icons

Monday, August 20, 2012

BARNABA KUMWANDIKIA 2FACE

Mwimbaji Barnaba atakua mwakilishi pekee wa Tanzania kupata mwaliko wa kwenda kuperform London U.K kwenye tamasha la wanamuziki mbalimbali wa nchi za Afrika ambao wanajitolea kuperform alafu zile pesa zinazopatikana zinarudi kwenye nchi zao kusaidia matatizo mbalimbali.
Kuhusu Barnaba kumuandikia mstari msanii 2face wa Nigeria, amesema “niko nae na nimepata bahati baada ya kutumiwa barua na wahusika kwamba nitaparform nae pamoja kwenye stage, katika vitu tutakavyofanya pamoja ni mimi kumuandikia chorus ya wimbo wake wa ‘African Queen’ kwa kiswahili aimbe na mimi nitaiimba chorus ya huo wimbo kwa kiingereza”
Mbali na 2Face, wasanii wengine watakaoperform kutoka Africa ni pamoja na D’banj na Mr Flavour na tamasha linafanyika London 27 August 2012 ambapo Barnaba anatarajia kuondoka siku yoyote kuanzia kesho.

No comments:

Post a Comment