Social Icons

Tuesday, December 18, 2012

UPELELEZI WA KESI YA LULU WAKAMILIKA

Ile kesi inayomkabili msanii wa Bongo Movie, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, jana imechukua hatua nyingine na inaonekana mshtakiwa huyo ameepuka adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa tuhuma za kumuua msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), alibadilishia mashtaka, ambapo awali mshtakiwa alisomewa mashtaka ya mauaji, lakini hadi kufikia jana katika mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu ilieleza kuwa upelelezi umekamilika na imeonekana mshtakiwa aliuwa bila kukusudia. Kutokana na mabadiliko hayo, Lulu ameepuka adhabu hiyo iliyokuwa ikimkabili kwani hata kama atapatikana na hatia, adhabu yake ni kifungo cha maisha au vinginevyo.
Kesi imeahirishwa tena hadi December 21 mwaka huu ili mshtakiwa aweze kusomewa muhtasari wa ushahidi na kisha jarada la kesi litafungwa na kesi itahamia Mahakama Kuu.

No comments:

Post a Comment