Social Icons

Thursday, December 13, 2012

STAMINA KUACHIA ALBUM YA KWANZA JANUARI

  Rapper wa muziki wa kizazi kipya anayewakilisha Moro Town, Stamina atarajia kuachia album yake mapema mwaka 2013. Stamina , mkali wa ngoma kama Kabwela, Alisema, Najuta Kubalehe na nyingine nyingi, alisema mitaa ya Januari fans wategemee album yake hiyo ambayo itakuwa  kwenye mtindo au miondoko ya Hip-Hop ikiwa imeshiba Track 22 ndani yake.

Stamina ambaye chimbuko lake ni Morogoro, aliyasema hayo jana na kuongeza kuwa, album hiyo imeshirikisha wasanii kibao kutoka bongo, kama Rich Mavoko, Fid Q, Mtu Chee na wengine kibao.


Katika hatua ingine, Stamina alisema single yake mpya aliyomshirikisha Fid Q inayojulikana kama Moto Moto ambayo teaser yake ilishatoka, hii itafuata kuiachia kwenye media kwa ajili ya fans wake na ipo katika hatua za mwisho za kuimalizia kuitengeneza na kwamba wakae mkao kwa zigo hilo ambalo yeye mwenyewe anasema ni kali sanaaa.

That's all new over Stamina, That tight MC from Moro Town u know....

No comments:

Post a Comment