kulikuwa na maneno mengi sana ya chichini mara baada ya kutolewa kwa video ya wimbo 'Baadae' wa mkali wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz ambayo kama wengi wanavyofahamu kichupa chake kiligongwa nje ya nchi.
kama ndiyo kwanza unasoma sentesi hii unaweza kujiuliza juu ya hicho ulichokisoma hapo juu, lakini ukweli ni kuwa nong'ono zilizokuwepo ni kuhusiana na msichana aliyetumika kwenye kichupa hicho kuonekana ni wa kiwango cha kawaida pengine kuliko hata warembo waliopo hapa nchini.
Taarifa zilizopo ni kuwa Ommy alitumia kiasi kikubwa cha fedha kusafiri mpaka nchini Afrika Kusini tayari kwa kufanya video hiyo huku pia akitumia mamilioni kumlipa msichana huyo ambaye licha ya kubeba sifa ya mmoja wa model maarufu nchini humo lakini bado hakuonekana kukidhi kiu ya watazamaji wa kichupa hicho
Hapo ndipo swali linapokuwa tunahitaji warembo wa kiwango gani kuzifanya video zetu kuwa za kuvutia zaidi, najiuliza ni wapi alipo Eliza yule aliyeshiriki kwenye video ya Bob Junior Oyoyo, ama ni wapi alipo yule binti aliyeonekana kwenye video ya Binti Kiziwi , si hao tu na imani kuna wengine wengi, sasa kama ni hivyo kun ahaja gani ya kusafiri mpaka ng'ambo kwenda kumchukua mtu ambaye uzuri wake haufanani hata na yule mwanamke mpenda sifa anayetangaza kipindi fulani cha runinga hapa nchini.
majibu tutayaona kupitia Comments zenu
No comments:
Post a Comment