Moracka kushoto akiwa na M. Kadinda
Ni kitambo sasa mkali wa 'Crank' Bongo, Mohamed Hassan Mo Racka amekuwa kimya jambo ambalo limekuwa likizusha nong'ono za hapa na pale kuwa huenda nyota huyo kafulia kimuziki.
Kupitia mchomvuink pekee stori iliyopo ni kuwa Mo anataraajia kukusanya mamilioni ya mkwanja kupitia matangazo ya kampuni moja kubwa hapa nchini dili ambayo kwa asilimia kuwa ndiyo ilimfanya kushindwa kufanya jambo lolote kwenye gemu ya Bongo fleva.
"Nitakupigia baada ya siku mbili uje kucheki mkataba wa mamilioni ambao ninatarajia kuusaini na kampuni moja kwa ajili ya matangazo, hilo ndiyo jambo lililokuwa linanifanya kuwa bize, nafikiri bada ya hapo nitakuwa poa kufanya kazi zangu za muziki kama kawaida" alisema Mo
No comments:
Post a Comment